10. Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,Na maarifa kuliko dhahabu safi.
11. Maana hekima ni bora kuliko marijani;Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
12. Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu;Natafuta maarifa na busara.
13. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;Kiburi na majivuno, na njia mbovu,Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
14. Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi;Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.
15. Kwa msaada wangu wafalme humiliki,Na wakuu wanahukumu haki.
16. Kwa msaada wangu wakuu hutawala,Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.