18. Haya, na tushibe upendo hata asubuhi,Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.
19. Maana mume wangu hayumo nyumbani,Amekwenda safari ya mbali;
20. Amechukua mfuko wa fedha mkononi;Atarudi wakati wa mwezi mpevu.
21. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi,Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22. Huyo akafuatana naye mara hiyo,Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni;Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23. Hata mshale umchome maini;Kama ndege aendaye haraka mtegoni;Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
24. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25. Moyo wako usizielekee njia zake,Wala usipotee katika mapito yake.