9. Ewe mvivu, utalala hata lini?Utaondoka lini katika usingizi wako?
10. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!
11. Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi,Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
12. Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu;Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu.
13. Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu,Huwaashiria watu kwa vidole vyake.
14. Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima,Hupanda mbegu za magomvi.
15. Basi msiba utampata kwa ghafula;Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona.
16. Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.