6. Ewe mvivu, mwendee chungu,Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7. Kwa maana yeye hana akida,Wala msimamizi, wala mkuu,
8. Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9. Ewe mvivu, utalala hata lini?Utaondoka lini katika usingizi wako?
10. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!