Mit. 27:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Usijisifu kwa ajili ya kesho;Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.

2. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe;Mtu mgeni wala si midomo yako wewe.

3. Jiwe ni zito, na mchanga hulemea;Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.

4. Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika;Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.

5. Lawama ya wazi ni heri,Kuliko upendo uliositirika.

6. Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

7. Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali;Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.

Mit. 27