Mit. 26:17-20 Swahili Union Version (SUV)

17. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake;Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.

18. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge,Na mishale, na mauti;

19. Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake,Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?

20. Moto hufa kwa kukosa kuni;Na bila mchongezi fitina hukoma.

Mit. 26