23. Upepo wa kusi huleta mvua;Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
24. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
25. Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu,Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali.
26. Mwenye haki amwangukiapo mtu mbayaNi kama chemchemi iliyochafuka,Na kisima kilichokanyagwa.
27. Haifai kula asali nyingi mno;Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.