30. Nalipita karibu na shamba la mvivu,Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31. Kumbe! Lote pia limemea miiba;Uso wake ulifunikwa kwa viwawi;Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32. Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana;Naliona, nikapata mafundisho.
33. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!