Mit. 23:6-12 Swahili Union Version (SUV)

6. Usile mkate wa mtu mwenye husuda;Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;

7. Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.Akuambia, Haya, kula, kunywa;Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.

8. Tonge lile ulilokula utalitapika,Na maneno yako matamu yatakupotea.

9. Usiseme masikioni mwa mpumbavu;Maana atadharau hekima ya maneno yako.

10. Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani;Wala usiingie katika mashamba ya yatima;

11. Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu;Atawatetea juu yako.

12. Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho;Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.

Mit. 23