Mit. 23:14-18 Swahili Union Version (SUV)

14. Utampiga kwa fimbo,Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

15. Mwanangu, kama moyo wako una hekima,Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu;

16. Naam, viuno vyangu vitafurahi,Midomo yako inenapo maneno mema.

17. Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi;Bali mche BWANA mchana kutwa;

18. Maana bila shaka iko thawabu;Na tumaini lako halitabatilika.

Mit. 23