6. Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongoNi moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.
7. Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali;Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.
8. Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana;Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.
9. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
10. Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu;Jirani yake hapati fadhili machoni pake.
11. Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima;Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa.