6. Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe;Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
7. Mwenye haki aendaye katika unyofu wake,Watoto wake wabarikiwa baada yake.
8. Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu,Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.
9. Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu;Nimetakasika dhambi yangu?
10. Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali,Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.