Mit. 2:10-17 Swahili Union Version (SUV)

10. Maana hekima itaingia moyoni mwako,Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;

11. Busara itakulinda;Ufahamu utakuhifadhi.

12. Ili kukuokoa na njia ya uovu,Na watu wanenao yaliyopotoka;

13. Watu waziachao njia za unyofu,Ili kuziendea njia za giza;

14. Wafurahio kutenda mabaya;Wapendezwao na upotoe wa waovu;

15. Waliopotoka katika njia zao;Walio wakaidi katika mapito yao.

16. Ili kuokoka na malaya,Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;

17. Amwachaye rafiki wa ujana wake,Na kulisahau agano la Mungu wake.

Mit. 2