1. Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu,Na kuyaweka akiba maagizo yangu;
2. Hata ukatega sikio lako kusikia hekima,Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3. Naam, ukiita busara,Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4. Ukiutafuta kama fedha,Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5. Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA,Na kupata kumjua Mungu.
6. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
7. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili;Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;