Mit. 19:9-12 Swahili Union Version (SUV)

9. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;Naye asemaye uongo ataangamia.

10. Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu;Sembuse mtumwa awatawale wakuu.

11. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake;Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.

12. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;Bali hisani yake kama umande juu ya majani.

Mit. 19