12. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
13. Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye;Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.
14. Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
15. Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;Na nafsi yake mvivu itaona njaa.
16. Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake;Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
17. Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA;Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
18. Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini;Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
19. Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake,Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena.