Mit. 11:28-30 Swahili Union Version (SUV)

28. Azitegemeaye mali zake ataanguka;Mwenye haki atasitawi kama jani.

29. Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo;Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.

30. Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima;Na mwenye hekima huvuta roho za watu.

Mit. 11