14. Wewe utashirikiana nasi;Tutakuwa na vitu vyote shirika.
15. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao;Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
16. Maana miguu yao huenda mbio maovuni,Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.
17. Kwa kuwa mtego hutegwa bure,Mbele ya macho ya ndege ye yote.
18. Na hao hujiotea damu yao wenyewe,Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.