1. Basi sasa, sikieni asemavyo BWANA; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako.
2. Sikieni, enyi milima, mateto ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana mateto na watu wake, naye atahojiana na Israeli.
3. Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa habari gani? Shuhudieni juu yangu.