8. Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasiopenda vita.
9. Wanawake wa watu wangu mwawatupa nje ya nyumba zao nzuri; watoto wao wachanga mwawanyang’anya utukufu wangu milele.
10. Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo mazito sana.
11. Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa.
12. Hakika nitakukusanya, Ee Yakobo, nyote pia;Bila shaka nitawakusanya waliobaki wa Israeli;Nitawaweka pamoja kama kondoo wa Bozra;Kama kundi la kondoo kati ya malisho yao;Watafanya mvumo kwa wingi wa watu;
13. Avunjaye amekwea juu mbele yao;Wamebomoa mahali, wakapita mpaka langoni,Wakatoka nje huko;Mfalme wao naye amepita akiwatangulia,Naye BWANA ametangulia mbele yao.