Mik. 2:4-9 Swahili Union Version (SUV)

4. Siku hiyo watatunga mithali juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema,Sisi tumeangamizwa kabisa;Yeye analibadili fungu la watu wangu;Jinsi anavyoniondolea hilo!Awagawia waasi mashamba yetu.

5. Kwa hiyo hutakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa BWANA.

6. Msitabiri, ndivyo watabirivyo; wasiyatabiri mambo haya; lawama hazikomi.

7. Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya BWANA imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu?

8. Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasiopenda vita.

9. Wanawake wa watu wangu mwawatupa nje ya nyumba zao nzuri; watoto wao wachanga mwawanyang’anya utukufu wangu milele.

Mik. 2