Mik. 1:6-14 Swahili Union Version (SUV)

6. Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake.

7. Na sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa-pondwa, na ijara zake zote zitateketezwa kwa moto, na sanamu zake zote nitazifanya ukiwa; kwa kuwa amezikusanya kwa ujira wa kahaba, nazo zitaurudia ujira wa kahaba.

8. Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia,Nitakwenda nimevua nguo, ni uchi;Nitafanya mlio kama wa mbweha,Na maombolezo kama ya mbuni.

9. Kwa maana jeraha zake haziponyekani;Maana msiba umeijilia hata Yuda,Unalifikia lango la watu wangu,Naam, hata Yerusalemu.

10. Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe;Katika Beth-le-Afra ugae-gae mavumbini.

11. Piteni; uende ukaaye Shafiri, hali ya uchi na aibu;Hivyo akaaye Saanani hajatokea nje;Maombolezo ya Beth-eseli yatawaondolea tegemeo lake;

12. Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema;Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa BWANA,Umefika mpaka lango la Yerusalemu.

13. Mfungie gari la vita farasiAliye mwepesi, ukaaye Lakishi;Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni;Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.

14. Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia;Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.

Mik. 1