12. Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema;Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa BWANA,Umefika mpaka lango la Yerusalemu.
13. Mfungie gari la vita farasiAliye mwepesi, ukaaye Lakishi;Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni;Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.
14. Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia;Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.
15. Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki;Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu.