5. Aishikaye amri hatajua neno baya;Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu.
6. Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa;
7. kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?
8. Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho;Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa;Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile;Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.