Mhu. 8:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Ni nani aliye kama mwenye hekima;Naye ni nani ajuaye kufasiri neno?Hekima ya mtu humng’ariza uso wake,Na ugumu wa uso wake hubadilika.

2. Mimi nasema hivi, Uishike amri ya mfalme; na hiyo kwa sababu umeapa kwa Mungu.

3. Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo.

4. Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?

Mhu. 8