Mhu. 4:9-14 Swahili Union Version (SUV)

9. Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11. Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12. Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

13. Heri kijana maskini mwenye hekimaKuliko mfalme mzee mpumbavu.ambaye hajui tena kupokea maonyo.

14. Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini.

Mhu. 4