Mhu. 12:8-10 Swahili Union Version (SUV)

8. Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!

9. Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi.

10. Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.

Mhu. 12