Mdo 12:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.

2. Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.

3. Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.

Mdo 12