Lk. 7:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.

2. Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.

3. Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.

4. Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili;

5. maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.

Lk. 7