Lk. 18:25-31 Swahili Union Version (SUV)

25. Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

26. Nao waliosikia walisema, Ni nani basi awezaye kuokoka?

27. Akasema, Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu.

28. Petro akasema, Tazama, sisi tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata.

29. Akawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu,

30. asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

31. Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii.

Lk. 18