4. na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.
5. Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.
6. Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu.
7. Kama akimtoa mwana-kondoo kuwa matoleo yake, ndipo atakapomtolea BWANA;
8. naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemsongeza, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.