Law. 3:11-14 Swahili Union Version (SUV)

11. Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

12. Na matoleo yake, kwamba ni mbuzi, ndipo atakapomtoa mbele za BWANA;

13. naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

14. Naye atasongeza katika sadaka hiyo matoleo yake, dhabihu kwa BWANA kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,

Law. 3