29. Tena mtakapomchinjia BWANA dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa.
30. Italiwa siku iyo hiyo; msisaze kitu chake hata asubuhi; mimi ndimi BWANA.
31. Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi BWANA.
32. Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi,
33. niliyewaleta mtoke nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA.