Kut. 37:23-28 Swahili Union Version (SUV)

23. Kisha akafanya taa zake saba, na makoleo yake, na visahani vyake, vya dhahabu safi.

24. Akakifanya cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo vyake vyote.

25. Kisha akafanya hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa moja, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa mbili; na pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo.

26. Naye akaifunika dhahabu safi, upande wa juu, na mbavu zake pande zote, na hizo pembe zake; akaifanyia na ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.

27. Naye akaifanyia vikuku viwili vya dhahabu na kuvitia chini ya ukingo wake, katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili, viwe ni mahali pa hiyo miti ya kuichukulia.

28. Kisha akafanya hiyo miti kwa mti wa mshita, na kuifunika dhahabu.

Kut. 37