Kut. 33:19-23 Swahili Union Version (SUV)

19. Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.

20. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.

21. BWANA akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba;

22. kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita;

23. nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.

Kut. 33