Kut. 32:34-35 Swahili Union Version (SUV)

34. Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.

35. BWANA akawapiga hao watu, kwa walivyoifanya ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.

Kut. 32