1. BWANA akanena na Musa, akamwambia,
2. Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.
3. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba,
4. na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani safi, na singa za mbuzi;