Kut. 2:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi.

2. Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.

3. Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto.

Kut. 2