Kut. 17:14-16 Swahili Union Version (SUV)

14. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.

15. Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;

16. akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

Kut. 17