Kum. 29:5-9 Swahili Union Version (SUV)

5. Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.

6. Hamkula mkate, wala hamkunywa divai, wala kileo; ili mpate kujua kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

7. Nanyi mlipokuja mahali hapa, walitutokea kupigana juu yetu Sihoni mfalme wa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, tukawapiga;

8. tukaitwaa nchi yao, nayo tukawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase, iwe urithi.

9. Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo.

Kum. 29