Kum. 29:25-29 Swahili Union Version (SUV)

25. Ndipo watakaposema watu, Ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri;

26. wakaenda wakatumikia miungu mingine, wakaiabudu miungu wasiyoijua, asiyowapa yeye;

27. ndipo ikawashwa hasira ya BWANA juu ya nchi hii, kwa kuleta juu yake laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki;

28. BWANA akawang’oa katika nchi yao kwa hasira, na ghadhabu, na makamio makuu, akawatupa waende nchi nyingine, kama hivi leo.

29. Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.

Kum. 29