Kum. 27:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza wale watu wakawaambia, Shikeni maagizo yote niwaagizayo leo.

2. Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo BWANA, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo,

3. uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi BWANA, Mungu wa baba zako.

4. Na iwe, mtakapokwisha vuka Yordani myasimamishe mawe haya, niwaagizayo hivi leo, katika mlima Ebali, nawe yatalize matalizo.

5. Na huko umjengee madhabahu BWANA, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.

6. Jenga hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee BWANA, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;

7. ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako.

Kum. 27