Wazaliwa wa kwanza waume wote wazaliwao katika kundi lako la ng’ombe na la kondoo, uwatakase kwa BWANA, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo.