Kum. 14:18-22 Swahili Union Version (SUV)

18. na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo.

19. Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.

20. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.

21. Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.

22. Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

Kum. 14