Isa. 63:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. Nalikanyaga shinikizoni peke yangu;Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu,Naliwaponda kwa ghadhabu yangu;Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao,Nami nimezichafua nguo zangu zote.

4. Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu,Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.

5. Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia;Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza;Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu,Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.

6. Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu,Nikawalevya kwa ghadhabu yangu,Nami nikaimwaga damu yao chini.

7. Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.

8. Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao.

Isa. 63