4. Inua macho yako, utazame pande zote;Wote wanakusanyana; wanakujia wewe;Wana wako watakuja kutoka mbali.Na binti zako watabebwa nyongani.
5. Ndipo utakapoona na kutiwa nuru,Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka;Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia,Utajiri wa mataifa utakuwasilia.
6. Wingi wa ngamia utakufunika,Ngamia vijana wa Midiani na Efa;Wote watakuja kutoka Sheba;Wataleta dhahabu na uvumba;Na kuzitangaza sifa za BWANA.
7. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali,Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.