1. Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?
2. Maana alikua mbele zake kama mche mwororo,Na kama mzizi katika nchi kavu;Yeye hana umbo wala uzuri;Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
3. Alidharauliwa na kukataliwa na watu;Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4. Hakika ameyachukua masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu;Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,Alichubuliwa kwa maovu yetu;Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.