Isa. 42:7-13 Swahili Union Version (SUV)

7. kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.

8. Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.

9. Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.

10. Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Na sifa zake tokea mwisho wa dunia;Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo,Na visiwa, nao wakaao humo.

11. Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao,Vijiji vinavyokaliwa na Kedari;Na waimbe wenyeji wa Sela,Wapige kelele toka vilele vya milima.

12. Na wamtukuze BWANA,Na kutangaza sifa zake visiwani.

13. BWANA atatokea kama shujaa;Ataamsha wivu kama mtu wa vita;Atalia, naam, atapiga kelele;Atawatenda adui zake mambo makuu.

Isa. 42