2. Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
3. Mimi, BWANA, nalilinda,Nitalitia maji kila dakika,Asije mtu akaliharibu;Usiku na mchana nitalilinda.
4. Hasira sinayo ndani yangu;Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu,Ningepanga vita juu yake,Ningeiteketeza yote pamoja.
5. Au azishike nguvu zangu,Afanye amani nami;Naam, afanye amani nami.
6. Siku zijazo Yakobo atatia mizizi;Israeli atatoa maua na kuchipuka;Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
7. Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?
8. Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.