Isa. 26:10-16 Swahili Union Version (SUV)

10. Mtu mbaya ajapofadhiliwa,Hata hivyo hatajifunza haki;Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,Wala hatauona utukufu wa BWANA.

11. BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

12. BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.

13. Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

14. Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.

15. Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

16. BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

Isa. 26